Mhe. Mchengerwa aipongeza timu ya wanawake ya Kriketi kwa kuongoza Rwanda

 


Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Tanzania ya  Wanawake ya Kriketi kwa kufanya vizuri na kuongoza kwenye mashindano ya Kwibuka Cup yanayoendelea nchini hivi sasa nchini Rwanda.

Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Juni 15, 2022 alipoongea na simu timu hiyo kupitia kwa Nahodha wa timu hiyo .

Amesema anaipongeza timu hiyo  baada ya kuzishinda timu zote walizokutana nazo kwenye mashindano hayo na kuwa kinalani mwa mashindano hayo.

Amezitaja timu hizo kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana na  Ujerumani  bado timu ya Nigeria na Brazil ambapo wakishinda mechi mojawapo wanaingia fainali za mashindano hayo.

Aidha, amemshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe.  Meja Jenerali Richard Makanzo  kwa kuwa karibu na timu hiyo katika kipindi chote huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili ifike mbali zaidi

Comments

Popular posts from this blog

Mhe. Mchengerwa- Serikali kuendelea kuwekeza kwenye timu zinazofanya vizuri, Gofu Wanawake, Twiga stars wanga'ra

MCHENGERWA AITAKA COSOTA KUTOA ELIMU YA KANUNI MPYA ZA ADA ZA VIBEBEA KAZI ZA SANAA NA MAKAMPUNI YA WASANII

MCHENGERWA AIPONGEZA WASAFI KWA KUKUZA VIPAJI VYA WASANII