Posts

Showing posts from August, 2022

Waziri Mchengerwa atoa wito kwa jeshi kuwa na timu ya soka.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ametoa wito  kwa majeshi kuanzisha  timu  ya soka itakayoshiriki ligi kuu nchini ili kuongeza ushindani na mvuto wa ligi. Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo usiku wa kuamkia leo Agosti 28, 2022 kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jakob John Mkunda katika uwanja wa Gofu wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akifunga  mashindano ya Gofu ya NBC Lugalo Patron Trophy 2022. Amefafanua kuwa majeshi yamekuwa na historia ya kutoa mchango mkubwa ambapo ameelezea kwamba   wachezaji wengi wanaoshinda katika mashindano mengi wanatoka kwenye majeshi. Aidha amesema kutokana na nidhamu iliyojengeka kwenye majeshi anaimani kuwa jeshi linauwezo wa kuanzisha timu hiyo ambayo itakuwa miongoni mwa timu tishio ndani na nje ya nchi yetu. Amesifu juhudi zinafanywa na jeshi katika kuanzisha klabu ya gofu na  miundombinu ya michezo huo Dar es Salaam na Dodoma na kuruhusu raia kutumia ambapo a...

Mhe. Mchengerwa ahesabiwa, asisitiza watu wote kuhesabiwa

Image
  Na John Mapepele, Rufiji . Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wanamichezo na wasanii wote kujitokeza kuhesabiwa  ili Serikali iweze  kupanga mipango ya maendeleo. Akiongea mara baada ya kuhesabiwa leo, Agosti 23, 2022 kwenye makazi yake Ikwiriri - Rufiji  amesema mafanikio ya kizazi cha kesho yatatokana na kujua idadi sahihi ya takwimu  za sasa. "Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa zoezi hili la sensa kwa kuwa  linalokwenda kutusaidia sana kuleta maendeleo" ameingeza Mhe. Mchengerwa Aidha, amesema sensa  ya mwaka huu ni muhimu  katika sekta za michezo, na sanaa kwa kuwa itasaidia  kupanga namna bora ya kuwahudumia watanzania kwenye sekta hizo. Amesema hiyo itasaidia kupanga namna na kujenga miundombinu  ya michezo kama vile viwanja vya michezo na  arena  za michezo. Amefafanua kuwa sensa itasaidia  mipango ya kibajeti kuandaa kanzi d...

Mhe. Mchengerwa awakabidhi Bendera Taifa Queens, awataka wafuzu Kombe la Dunia.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakabidhi Bendera yaTaifa timu ya Taifa ya Netiboli ya Taifa Queens kama ishara ya kuwaaga kwenda kwenye mashindano ya kufuzu kushiriki Kombe la dunia yanayofanyika nchini Afrika Kusini. Akikabidhi bendera hiyo leo Agosti 18, 2022 jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amewataka   kutanguliza uzalendo na utaifa katika mashindano hayo ili kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia kwenye mashindano ya dunia.  “Naomba niwaambie ndugu zangu nnyie mnaweza kabisa kuandika historia ya kuwa timu ya tano katika nchi yetu kuingia kwenye mashindano ya dunia endapo mtakuwa wazalendo, nendeni mkacheze kufa na kupona kama ni kuvunjika mkavunjikie uwanjani lakini mrudi na ushindi nyumbani, nasi tutawapokea kwa heshima kubwa” Amefafanua Mhe. Mchengerwa. Aidha, amewataka watambue kuwa wakifanya vizuri watakuwa wamefungua ukurasa mpya wa maisha yao kwa kuwa timu kubwa duniani zitawanunua kitu ambacho k...

Tanzania na Falme za Kiarabu waja na tamasha kubwa la Utamaduni

Image
  Na John Mapepele Tanzania kwa kushirikiana na  nchi zote za falme za kiarabu inatarajia kufanya  tamasha kubwa la Utamaduni Februari mwakani jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na leo Agosti 18, 2022 na  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Qatar nchi, Mhe. Husain Ahmad Al- Homaid aliyeambatana na ujumbe kutoka nchini Kuwait. Aidha, amefafanua kuwa nchi hizo kabla ya uamuzi huo walitafiti na kuona kuwa  Tanzania imebarikiwa kuwa na Utamaduni tofauti na nchi nyingi duniani, hivyo kufanya tamasha hilo la pamoja litakuwa na faida kubwa kwa pande zote mbili. Amesema maonesho  hayo ni maalum ya kiutamaduni ambapo yatajikita katika Sanaa za uchoraji, uchongaji pamoja na nyimbo. Ameongeza kuwa Utamaduni na sanaa za Tanzania zina historia ndefu katika ukombozi wa Bara la Afrika ambapo amesisitiza kuwa Baba wa taifa wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere aliwaunganisha watanzania hadi kupata uhuru k...

Waziri Mchengerwa aelekeza vilabu vyote kumiliki viwanja vyake vyenyewe, Yanga na Simba vyaahidi kutekeleza agizo hilo ndani ya miezi sita

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Agosti 17, 2022 ameelekeza vilabu vyote kumiliki viwanja vyake vyenyewe ambapo timu ya  Yanga na Simba zimeahidi kutekeleza agizo hilo ndani ya miezi sita.  Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo  alipokutana na  watendaji wakuu wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu  jijini Dar es Salaam na  kujadili  namna bora ya kuendesha ligi   kwa ubunifu na ushindani wa hali ya juu ili kuifanya ligi iwe na mvuto. Mhe. Mchengerwa amesema mpango wa vilabu kumiliki  viwanja vyao  ni takwa la kisheri kulingana na Sera ya Michezo nchini. Aidha, Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa  pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili masuala ya kuzingatia  weledi, nidhamu na maadili. Amesema kwa sasa Serikali haiwezi kukubaliana na vitendo vyovyote vya rushwa na upendeleo katika michezo kwa kuwa vinasaidia kuua na kudidimiza michezo. Amesema dhamira ya Serikali  kwa ...

KUPOKEA TAARIFA YA KUSIMAMIA HAKIMILIKI NA UGAWAJI WA MIRAHABA NA MASHUJAA WA JUMUIYA YA MADOLA

Image
                       Na Mwandishi wetu– Dodoma  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa kesho Agosti 12, 2022, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kupokea  taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Ugawaji wa  Mirahaba kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa ya Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzia saa 11 jioni jijini Dar es Salaam.  Uteuzi wa Kamati hiyo, ulitokana na malalamiko ya wadau hususan wa Sekta ya  Sanaa nchini kuhusiana na namna mirabaha inavyokusanywa na kugawanywa,  kuwepo kwa vitendo vya uharamia katika kazi zao na elimu duni kwa wadau  kuhusu masuala hayo.  Aidha, uundaji wa Kamati hiyo ulitokana na maelekezo ya Mhe. Rais ya  kuitaka Wizara kusimamia na kutafuta muarobaini wa changamoto za  mirabaha kwa wasanii aliyoitoa Mei 30, 2022 jijini Dar es ...

Waziri Mchengerwa awaongoza Rais wa FIFA, nchi 58 kuitazama Royal Tour

Image
  Na John Mapepele, Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, usiku wa Agosti 10, 2022 amewaongoza viongozi wakuu wa nchi 58 wa mashirikisho ya Soka kuangalia Filamu ya Royal Tour jijini Arusha. Mhe. Mchengerwa amewaongoza kutazama  filamu hiyo iliyochezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia  Suluhu Hassan ambayo imewavutia  wengi kuiangalia na kuomba kutembelea maeneo mbalimbali. Tayari makundi matatu ya washiriki yamejitokeza kutembelea Hifadhi za Ngorongoro, Serengeti na Zanzibar kuanzia kesho Agosti 11, 2022. Kundi hili la viongozi limewajumuisha takribani watu mia tano ambao ni washiriki wa mkutano mkuu wa Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) ambao wamemaliza mkutano wao wa siku mmoja uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha  Mikutano cha Arusha. Mhe.  Mchengerwa amewakaribisha washiriki wote kutembelea vivutio vya utalii ambavyo Tanzania imebarikiwa ambavyo havipatikani sehemu nyingi duniani. Aidha, amewashukuru Rais wa Shir...

Mhe.Mchengerwa ampokea Rais wa FIFA

Image
  Na John Mapepele, Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku huu ameongoza ujumbe wa kumpokea Rais wa FIFA Gianni Infantino anayekuja kuhudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la  Soka Barani Afrika (CAF). Mkutano huo wa kwanza wa kihistoria unafanyika kwa mara ya kwanza nchini huku zaidi ya nchi 58 kutoka sehemu mbalimbali duniani zikishiriki. Mhe. Mchengerwa amemkaribisha  Rais wa FIFA Gianni na kumpatia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumwelezea  jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ambapo Rais wa FIFA ameelezwa kuridhishwa na maendeleo ya Michezo. Amepongeza kazi kubwa huku akisema amefurahishwa na makaribisho hayo. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na kuangaliwa na watu zaidi ya bilioni moja. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Mhe. Rais. Katika mkutano huo CAF inakwenda kuzindua  mashindano maalum ya soka y...

MHE. MCHENGERWA - CAF KUZINDUA “AFRIKA SUPER CUP

Image
  Na John Mapepele- Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Omary Mchengerwa amesema Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) unaofanyika kesho Agosti 10,2022 jijini Arusha Tanzania, unakwenda kuzindua mashindano maalum ya kandanda ya Afrika Super CUP. Akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Arusha leo, Agosti 9, 2022 Mhe. Mchengerwa amesema mkutano huo ambao ni wa kwanza wa kihistoria katika Bara la Afrika na Tanzania unafaida kubwa kiuchumi na kimichezo.  Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa baadhi ya wageni wanaoshiriki kwenye mkutano huo wameshapanga kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii hapa nchini baada ya kumalizika kwa mkutano huo. Mchengerwa amesema mkutano huo wa 44 unatarajiwa kufanyika kesho ambapo unajumuisha mataifa 58 na nchi 54 ni za Afrika. Aidha, amesema ni nchi mbili tu za Afrika yaani Kenya na Zimbabwe ambazo zinatumikia adhabu ambazo hazishiriki kwenye mkutano huo. Amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na Rais wa CAF Dkt....

Waziri Mchengerwa akutana na UNESCO, aunda tume ya uanzishwaji wa chuo Kikuu cha Kiswahili

Image
  Na John Mapepele,  Waziri wa Utamaduni, Sanaa Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana  na ujumbe wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameunda tume kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiswahili nchini ikiwa ni mkakati kabambe wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili  katika  mabara yote duniani. Mhe, Mchengerwa ameunda tume maalum ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kiswahili kufuatia  ombi lake alilolitoa  kwa  shirika  la UNESCO wakati wa siku ya  maadhimisho ya Kiswahili duniani   mwaka huu iliyofanyika  kwa mara ya  kwanza  Julai 7, 2022.  Akizungumza mara baada ya mkutano na ujumbe wa UNESCO ofisi za Tanzania leo Agosti 5, 2022 ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema matajio ya  Serikali ni kuona kuwa Kiswahili kinavuka mipaka  ya   Tanzania. Aidha, Mhe Mchengerwa ameipa tume  hiyo siku  tano  kukamilisha andiko  hilo ili liwasi...