Mhe. Mchengerwa- Serikali kuendelea kuwekeza kwenye timu zinazofanya vizuri, Gofu Wanawake, Twiga stars wanga'ra
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwenye timu zinazofanya vizuri huku akiwataka Watendaji wa michezo kufanya tathmini kwa zisizofanya vizuri ili Serikali ichukue maamuzi magumu. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya usiku wa leo hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa mashindano ya Afrika ya Gofu ya Wanawake -All Africa Competition Trophy (AACT) yaliyofanyika kuanzia Septemba, 6-8, 2022 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na kushirisha nchi 20. Katika mashindano hayo Tanzania imeshika nafasi ya tatu wakati Morocco imeshika nafasi ya pili na nchi ya Afrika Kusini kuwa mshindi wa kwanza. Ameipongeza timu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya tatu huku akifafanua kuwa hayo ni matunda ya uwekezaji mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye michezo katika kipindi kifupi cha uongozi wake. Aidha, ameipongeza timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Twiga Stars kwa ku...

Comments
Post a Comment